Neema Gospel Choir
780 subscribers
91 photos
68 videos
2 files
85 links
Born again Christians | Singers | Members of Africa Inland Church Tanzania ๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ(AICT) | Chang'ombe - Dar es salaam
Download Telegram
Tunamshukuru Mungu aliyekuwa pamoja nasi tangu mwanzo wa safari yetu mwaka 1992 na leo tunatimiza miaka 29 katika huduma.

Haikuwa rahisi kufika hapa, kwa Msaada wa Mungu bado ametukusanya pamoja na kuendelea kuilinda huduma yake.

Tunawashukuru sana Wote mnaotuombea kwa ajili ya kusupport huduma yetu. Wale mnaojitoa kwa Maombi, Mali, Pesa hata Muda kwa ajili ya Huduma yetu.

*Bwana kwa nguvu zako, Hatutadhurika. Kwa vitu vya kufisha, Hatutadhurika*

Mbarikiwe wote.
Channel photo updated
BEI ZA T-SHIRT

SHORT SLEEVE (Mikono mifupi) Tsh - 20,000/-
Rangi (White, Maroon, Black, Grey)

LONG SLEEVE (Mikono Mirefu) Tsh - 25,000/-
Rangi (White, Maroon, Black, Grey)

HOODIE (Pool-over - Sweta ) Tsh - 25,000/-
Rangi (White, Maroon, Black, Grey)

Kupata Tshirt yako - Piga simu: +255 755 471 133 (Robert)
Tunakutumia Popote ulipo!

Hizi ni T-Shirt Maalum kwa ajili ya kumuandalia Mungu ibada Tar 03 December, Sadaka yako ya Kununua T-Shirt itafanikisha ibada hiyo.
Karibu, Ujiunge nasi, Katika kusauport kazi ya Mungu kwa sadaka hii,

Unarikiwe!
Leo tutaanza kuachia Track list nzima inayobeba Album mpya ya #TheSoundOfAhsante Kaa tayari, Huku ukiombea kazi hii,
Rasmi itakuwa released Jumapili 10 October 2021.

Kuelekea Live Recording yetu 03 December

#neemagospelchoir #worshipinspirit #NewAlbum #release #2021
AHADI
Ni wimbo wa ushuhuda wa Matendo makuu ya Mungu, ni wimbo mahususi kukupa nguvu na ujasiri kuwa Mungu hufanya ufumbuzi wa shida zetu kwa wakati sahihi kwake.

2 Wakorintho 1:20
Maana ahadi zote za Mungu zilizopo katika yeye ni Ndiyo; tena kwa hiyo katika yeye ni Amin; Mungu apate kutukuzwa kwa sisi.

Huu ni moja kati ya nyimbo zinazoiunda Album yetu mpya ya THE SOUND OF AHSANTE
Itatoka Rasmi Tar 10 October 2021
NEEMA YA MUNGU
Wimbo wa shukurani juu ya ukombozi.
Karama ya Mungu ni upendo usiomithilika. Kupitia Yesu, ametukomboa; si kwa matendo yetu bali kwa upendo na huruma yake.
Tunapaswa kumshukuru Mungu kwa neema ya wokovu.

Efeso 2:8-9
Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; na si kwa sababu ya matendo yenu mema. Hii ni zawadi kutoka kwa Mungu mwenyewe. Na kwa sababu hamkuifanyia kazi, mtu yeyote asije akajisifu juu ya wokovu wake.

Huu ni moja kati ya nyimbo zinazoiunda Album yetu mpya ya THE SOUND OF AHSANTE
Itatoka Rasmi Tar 10 October 2021
ENYI WATUMISHI
Kuenenda katika utauwa/usafi wa moyo ndio msingi wa kumpendeza Mungu.
Ahadi ya Mungu ni kutulinda na kukaa ndani yetu iwapo tutamtii.

Isaya 52:11-12
Nendeni zenu, nendeni zenu, tokeni huko, msiguse kitu kichafu; tokeni kati yake; iweni safi ninyi mnaochukua vyombo vya Bwana.
Maana hamtatoka kwa haraka, wala hamtakwenda kwa kukimbia, kwa sababu Bwana atawatangulia; na Mungu wa Israeli atawafuata nyuma; awalinde.

Huu ni moja kati ya nyimbo zinazoiunda Album yetu mpya ya THE SOUND OF AHSANTE
Itatoka Rasmi Tar 10 October 2021
*NURU YA ULIMWENGU*
Wito maalum kwa watu wote walio okoka ni kuyatenda yaliyomema ili watu wengine ambao hawajaokoka wajifunze na kuona uzuri wa wokovu kupitia matendo yetu.

1Petr 1:15-16,
15 Bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, kadhalika ninyi muwe watakatifu katika mwenendo wenu; 16 maana imeandikwa: โ€œMuwe watakatifu kwa sababu mimi ni mtakatifu.โ€

Mathayo 5:14-16
14 โ€œNinyi ni nuru ya ulimwengu. Mji uliojengwa kwenye mlima haufichiki. 15 Wala hakuna mtu anayewasha taa kisha akaifunika. Badala yake, huiweka mahali pa juu ili itoe mwanga kwa kila mtu aliyemo ndani ya nyumba. 16 Hali kadhalika, nuru yenu iwaangazie watu ili waone matendo yenu mema wamtukuze Baba yenu aliye mbin guni.โ€™

Huu ni moja kati ya nyimbo zinazoiunda Album yetu mpya ya *THE SOUND OF AHSANTE*
Itatoka Rasmi Tar 10 October 2021
Kaa tayari... Tsh 20,000/=