Umoja wa Walimu Wasiokuwa na Ajira Tanzania (NETO), wameamua kuingia kwenye maombi ya siku tatu, kumuomba Mungu, ili serikali itoe majibu yenye kuleta ahueni kwa wasio na ajira nchini.
Hatua hiyo, imetajwa kuwa ni kutokana na kuwa wanaelekea ukingoni mwa siku 45 zilizowekwa na serikali kusubiri hatma ya NETO, ikiwa leo ni siku ya 18.
Naibu Katibu wa NETO, Yasinta Mcharo, kupitia ukurasa wao wa WhatsApp Chanel amesema mfungo huo unaanza kesho Aprili 9 hadi 11,2025 na kwamba mfungo huo ni kwa kila mmoja na dini yake.
"Leo Bunge la bajeti limeanza hivyo Mungu awafanyie wepesi viongozi bungeni kuongeza Bajeti ya kuajiri walimu wengi zaidi nchini, ili tupate fursa ya ajira kwa walimu wote," amesema.
Machi 12, 2025, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene alikutana na NETO na kuahidi serikali itaunda timu ya wataalam kutoka wizara tano, ili kushughulikia jambo hilo. Iliahidi itatoa taarifa ndani ya kipindi cha mwezi hadi siku 45
Imeandikwa na Beatrice Moses, Dar es Salaam
#nipashedigital #nipasheupdates