TCRA imezitaja sababu za data kuisha haraka kuwa ni kuongezeka kwa speed ya Mitandao na uwezo wa Smartphone na kuongezeka kwa ukubwa wa App nyingi zinazotumika kuwa na update za mara kwa mara na kuongezeka kwa quality ya picha na video ambazo zinaongeza ukubwa.
#MillardAyoUPDATES
#MillardAyoUPDATES
Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Moshi Jonathan Kabengwe, amesema majina ya Waombaji wa ajira 1,596 zilizotangazwa na TRA hivi karibuni yatatangazwa rasmi kesho March 22 2025 kupitia tovuti ya TRA (www.tra.go.tz) kwa ajili ya usaili wa kuandika utakaofanyika March 29 na 30 mwaka huu kwenye Vituo 9 tofauti vya Tanzania bara na Visiwani.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es salaam leo tarehe 21.03.2025, Kabengwe amesema kati ya Waombaji 135,027 waliotuma maombi ya nafasi hizo za ajira, Waombaji 112,952 wamekidhi vigezo na kuitwa kwenye usaili wa kuandika ambapo sasa kila Muombaji atatumiwa katika barua pepe yake taarifa ya kuitwa kwenye usaili ambapo pia Waombaji wenye mahitaji maalum watawekewa utaratibu maalum ambao utawasaidia kufanya usaili bila usumbufu.
Kabengwe amesisitiza kuwa Waombaji wote watatendewa haki na kwamba usaili huo utafanyika kwenye Mikoa 8 ya Tanzania Bara na kwa Visiwani Zanzibar usaili utafanyika Unguja na Pemba kama inavyoonekana kwenye orodha ifuatayo.
1. Dar es salaam ambayo itahusisha Waombaji kutoka Dar es salaam na Pwani.
2. Zanzibar ambayo itahusisha Waombaji kutoka Unguja na Pemba
3. Arusha ambayo itahusisha Waombaji kutoka Arusha, Manyara, Kilimanjaro na Tanga.
4. Dodoma ambayo itahusisha Waombaji kutoka Morogoro, Dodoma, Singida, Iringa na Tabora
5. Mtwara ambayo itahusisha Waombaji kutoka Mtwara, Lindi na Ruvuma
6. Mbeya ambayo itahusisha Waombaji kutoka Mbeya, Songwe na Rukwa
7. Mwanza ambayo itahusisha Waombaji kutoka Mwanza, Shinyanga, Mara na Simiyu.
8. Kagera ambayo itahusisha Waombaji kutoka Kagera na Geita.
9. Kigoma ambayo itahusisha Waombaji kutoka Kigoma na Katavi.