NAFASI ZA KAZI & NEWS CHANNEL
61 subscribers
1 photo
113 links
Pata Habari na Matukio Mbalimbali yanayotokea kila siku Nchini Tanzania na Duniani kwa ujumla zikiwepo nafasi Mpya za Kazi Kwenye Taasisi za Umma na Sekta Binafsi
Download Telegram
📌 DKt Biteko afungua rasmi, aishukuru PAC kwa mchango wao sekta ya Nishati

📌 Waitaka TPDC kuwekeza kwa kutumia fedha za ndani na sio kutegemea wafadhili pekee

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Biteko ameipongeza kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za serikali (PAC) kwa kusimamia na kushauri vema mashirika yanayotekeleza miradi mbalimbali ya serikali, kwani wamekuwa wakitoa mchango mkubwa kwenye mafanikio ya miradi hiyo.

Dkt. Biteko ameyasema hayo wakati akifungua semina ya kamati ya Bunge ya PAC iliyoandaliwa na Wizara ya Nishati kupitia Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC) wakati wakiwasilisha mpango wa bajeti ya miradi ya maendeleo itakayotekelezwa na TPDC kwa mwaka wa fedha 2024/2025.*

https://www.masamablog.com/2024/06/tpdc-yatakiwa-kufanya-haya-muhimu-na.html?m=1
*Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara za Minini na Vijiji ni (TARURA) Mhandisi Victor Seff amesema Wakala Hiyo inaendelea na kazi za matengenezo na ufunguaji wa Barabara Mpya kadri inavyoweza kwani ni moja ya Malengo yake kwa mwaka huu wa Fedha wa 2024/2025 kama ilivyokuwa mwaka jana wa fedha wa 2023/2024 na miaka ya nyuma .*

*Aidha Mhandisi Seff amesema kazi za ujenzi zinaendelea Mikoa mbalimbali kazi zinaendelea ikiwa ni moja ya utekelezaji wa Maelekezo ya Serikali ya awamu ya Sita Chini ya Mhe Rais Dkt. Samia Sauluhu Hassan ya kuhakikisha wananchi wanaboreshewa miundombinu ili waweze kujikwamua kiuchumi kwa kuongeza kasi ya maendeleo.*

https://www.masamablog.com/2024/07/jionee-baadhi-ya-kazi-zilizofanywa-na.html